|
SHEREHE
Ngoma hii inaitwa kiini macho. Huchezwa katika sherehe za mazingaombwe, yaani kupunga pepo.
Zamani ngoma hizi hazikuwa zikichezwa na kila mtu. Zilichezwa na wenyeji wa
Pemba au wakaazi wa sehemu za mashambani Unguja. Baada ya mapinduzi katika
kisiwa cha Unguja, mapinduzi ambayo yaliondoa utawala wa
waarabu, ngoma hizi zilianza kuchezwa katika sherehe za kisiasa.
Nia yake ilikuwa kudumisha na kuonyesha umuhimu wa utamaduni wa Wazanzibari
katika siasa ya nchi. Kwa hivyo, watu kutoka katika sehemu mbalimbali za Zanzibar
wanajifunza ngoma hizi. Ngoma hizi sasa zimeshika nafasi ya kitaifa badala
ya jadi peke
yake. Wachezaji hawa ni kikundi cha taifa cha utamaduni Zanzibar. Ni
sehemu ya wizara ya elimu ya taifa. Kwa hivyo, wanawawakilisha Wazanzibari
wote na sio kikundi maalum cha
Wazanzibari.
|