|
KULA MGAHAWANI
Kwa desturi, watu wengi hupendelea kula
chakula kilichopikwa nyumbani. Kama tulivyoona katika somo la kwanza na somo
la pili, uhusiano wa kifamilia ni muhimu sana katika utamaduni wa waafrika. Familia
hukaa pamoja na kula chakula cha siku pamoja. Kwenda mgahawani ni namna ya kujistarehesha.
Mara moja moja, familia, au mmoja wa familia anaweza kwenda mgahawani kula na
kunywa na marafiki. Wakati huu hupata nafasi ya kukutana na watu wengine, kupashana habari
na kuzungumza mambo mengi ya siasa na maisha. Kwa sehemu kubwa ni wanaume wanaokwenda
mgahawani kula na kunywa. Wanawake wengi hawawezi kwenda mgahawani mara
kwa mara kwa sababu ya wajibu wao
katika familia. Wanaweza kwenda wakati wa sherehe au siku za mapumziko ya kazi
kama Jumapili, au sikukuu za dini na serikali.
|