Home
Overview
Technical Help

Select Unit > Unit 12: Uganga wa jadi > Lesson 1:

    

WAGANGA WA JADI

Wagonjwa wengi huwategemea waganga wa jadi. Kuna sababu tatu maalum. Moja, waganga wa jadi waliwatibu watu walioishi katika vijiji vyao kabla ya huduma za afya za kisasa kuanzishwa katika vijiji. Mbili, watu wengi bado wanakaa mbali na vituo vya afya, kwa hivyo waganga wa jadi wanaendelea kutoa matibabu ya awali kwa wagonjwa katika jamii zao. Tatu, baadhi ya wananchi wanaamini zaidi matibabu ya jadi. Hutafuta matibabu ya kisasa kama mganga wa jadi anashauri hivyo. Leo tulawatembelea waganga mbalimbali na kuona shughuli zao.

Karibuni katika uganga wa jadi. Hiki ni kituo cha Kilingemoto. Huyu ni mganga wa kituo na hawa wasaidizi wake. Pamoja na kutibu wagonjwa katika kituo hiki, mganga huyu huwafundisha vijana juu ya utamaduni wao wa uganga wa jadi.

© African Studies Institute, University of Georgia.