MGANGA MAGWAYA
Sasa
tutamtembelea mganga mwingine. Jina lake ni mganga Magwaya. Matibabu
yake ni tofauti na mganga Hamisi wa Kilingemoto. Mganga Magwaya
anatumia imani za miungu pamoja
na dawa nyingine za jadi ili kutibu wagonjwa wake. Mganga Hamisi
anatumia miti
shamba tu. Karibuni nyumbani kwa mganga Magwaya. Katika mazungumzo
ni profesa Mshiu wa taasisi ya madawa ya asili, chuo kikuu cha
Dar-es-salaam.
Profesa: Babu tunapenda kufahamu jina lako ni nani?
Mganga: Jina langu ninaitwa Mkwayu, mganga wa kienyeji. Ni
mganga wa jadi. Kwanza uzazi,
pili mbavu, kifua,
mtu anayetapika damu,
au kuvimba.
Kwa hivyo ndivyo vigonjwa ninavyotumikia na maradhi
ya kichaa, yaani mawewe hayo.
Profesa: Mawewe?
Mganga: Eeeh, kichaa, hayo ni mawewe. Hayo ndio wagonjwa ninaohudumia kwa masaa yote.
|