KITUO CHA AFYA ILALA
Leo tutatembelea kituo cha afya cha Ilala. Ilala ni wilaya mojawapo katika mkoa wa Dar-es-salaam. Kutoka mjini Dar-es-Salaam hadi Ilala ni umbali wa maili tatu hivi. Katika kituo hicho tutamtembelea daktari mkuu msaidizi wa kituo. Jina lake ni daktari Senge.
Hii ni sehemu ya mafunzo na matibabu ya mama wajawazito. Hapa wanapimwa uzito, damu, mkojo, mapigo ya moyo, shinikizo la damu na uvimbe katika viungo vya mwili.
Mganga: Hii ni sehemu ambayo tunatoa huduma za mama
wajawazito. Akina mama wanakuja wanapokuwa
na mimba kuanzia miezi miwili. Tunawashauri waanze
kuja mpaka wanapojifungua.
Hapa mama mjamzito anapimwa uzito. Hapa mama mjamzito anapimwa shinikizo la damu na uvimbe katika miguu. Baada ya kujifungua, akina mama hawa wanapewa mafunzo ya afya na hasa juu ya uzazi wa majira.
|