|
WADI YA WATOTO
Kama alivyosema daktari Senge, baadhi ya wagonjwa hulazwa hapa kituoni. Kama
ni wagonjwa zaidi, hupelekwa katika hospitali kuu ya mkoa wa Dar-es-Salaam,
yaani hospitali ya Muhimbili. Katika wadi ya watoto kuna watoto wagonjwa wachache.
Mtoto huyu ana jipu mkononi.
Kwa kawaida kama mtoto analazwa hospitalini, mama mzazi au ndugu anakaa hospitali
kumhudumia. Hapa tunamuona daktari wa watoto, daktari Limo katika wadi ya watoto.
Atajulishwa na daktari Senge na baadaye atatueleza kidogo juu ya wadi hii na
kazi zake.
Mtoto huyu ni mgonjwa sana. Ana homa kali ya malaria. Ili kupunguza joto la homa yake, nesi anamkanda mwili wote kwa maji ya baridi sana. Mtoto huyu alikuwa na homa kali pia. Lakini sasa ana nafuu na amelala. Mama yake anatumaini kwamba wataruhusiwa kurudi nyumbani hivi karibuni.
|