TAASISI YA MADAWA YA ASILI
Kiungo baina ya tiba za jadi na tiba za kisasa ni Taasisi ya madawa ya asili. Hii ni sehemu ya chuo kikuu cha Dar-es-Salaam, kitivo cha tiba, Muhimbili. Utafiti wa madawa ya jadi katika Taasisi hii ulianza 1972. Kuna watafiti ambao kazi zao muhimu ni kuchunguza miti shamba ili kupata madawa mbalimbali.
|