|
SHUGHULI ZA TAASISI
Taasisi
ya madawa asilia ina maabara ya
baolojia na kemia ya mimea. Pia taasisi hufanya utafiti katika
famakolijia na toksikolojia kwa kutumia miti shamba. Madhumuni
ya utafiti katika maabara haya ni kuhakikisha kwamba
dawa wanazotumia waganga wa jadi zinafanya kazi sawa
sawa. Pia wanawasaili waganga
wa jadi, wanaweka kumbuku za idadi ya waganga wa jadi, na wanaweka
kumbukumbu za shughuli za waganga wa jadi. Taasisi inategemea kwamba
itaweza
kutengeneza
madawa katika
maabara
ya Tanzania. Itaweza kuanzisha famasia za madawa ya jadi sehemu
mbalimbali katika nchi. Pia Taasisi ina jukumu la
kuwafundisha wananchi juu ya umuhimu wa kuhifadhi mimea asili
na kuotesha mimea ya dawa mbali mbali. Taasisi ina wataalamu wa
anthropojia ambao wanafanya utafiti juu ya desturi na mila za waganga.
Majani haya ni ya mti unaoitwa muarubaini. Inasemekana ni dawa
ya malaria.
|