Home
Overview
Technical Help

Select Unit > Unit 13: Desturi za Arusi > Lesson 3: Hide transcript

    

KUMWAGA BIBI ARUSI

Nakukabidhi huyu dada yangu akaishi na mume wake salama starehe. Hana kovu na wala hajakonda. Endapo kama mume wake atamshinda amrudishe kwangu kama alivyo. Kwa hivyo huyu dada yangu.

Sasa binti arusi amekaa juu ya kigoda na mshenga wake.

Sasa bwana arusi anakaribishwa ili yeye na binti arusi wapewe baraka za ukoo.

Kuonyesha mchanganyiko wa desturi, mila na tamaduni mbalimbali, wageni wanatumbuizwa kwa nyimbo za taarab na ngoma za jadi. Nyimbo zinasisitiza sifa za binti arusi, umuhimu wa familia na upendo baina ya mume na mke.

Mwimbaji taarab anampa wosia binti juu ya heshima kwa wakwe zake na watu wa famila.

African Languages Program, University of Georgia