Home
Overview
Technical Help

Select Unit > Unit 13: Desturi za Arusi > Lesson 4: Hide transcript

    

BIBI ARUSI ANAPEWA WASIA

Katika sherehe hizi pia, familia ya binti arusi humpa wasia. Yaani ushauri wa jinsi ya kuishi na mume wake na wakwe zake, heshima kwa wakwe na matunzo bora ya familia yake. Kwa niaba ya baba mzazi, baba mdogo wa binti arusi anampa wasia.

Asante sana ndugu zangu, ndugu zangu wakaribishwa. Sasa hivi kitu ambacho tunamalizia kilele cha sherehe hii ya mkesha tunasema ni mtiririko wa kumtoa binti arusi ndiyo kilele cha sherehe yenyewe. Mimi nafananisha kama ni mahafali kama alivyoimba huyo binti wa taarab ni kama mtoto wetu amefikia wakati ambao sisi tunaona kwamba amejifunza katika maisha ya mwanadamu. Amejifunza vitu vingi sana chuoni baadhi ya vitu ambavyo amejifunza chuoni vimechukua muda mrefu kupata shahada, stashahada lakini kuweza kufuzu na kuwa tayari kuingia katika maisha ya ndoa ni kozi ambayo inachukua muda mrefu. Kwa kweli imeanza wakati mtoto anapozaliwa inaendelea kwa miaka mingi. Wakati huu anapata mihadhara mingi. Siyo mizuri kwake. Hayapendelei (mambo ya mihadhara). Lakini anayasikiliza na akifuata hatua zinazopendekezwa na wazazi wake pamoja na matendo ambayo ameonyeshwa na anaweza kufikia hatua ambayo binti yetu amefikia. Kwa hivyo sasa hivi tumefurahi kwamba amefikia wakati ambao tunaweza kusema hana matatizo yoyote. Ameshafuzu. Hatuna waswasi naye.

African Languages Program, University of Georgia