Home
Overview
Technical Help

Select Unit > Unit 14: Mapishi > Lesson 1: Hide transcript

    

Wanawake wa familia ya Mzee Ayubu Wanapika

Dada Aisha anafanya nini sasa? Anatwanga kisamvu, yaani majani ya mhogo. Anatumia mchi na kinu. Baada ya kutwanga kwa muda, anakichota kisamvu na anakipeleka jikoni kuanza kukipika.

Dada Zainabu anatayarisha nazi. Kwanza anaipara nazi. Kisha anaipasua. Sasa anaikuna kwa kutumia mbuzi. Atachanganya machicha yake maji ili kutengeneza tui la kupikia vyakula mbalimbali.

Dada Aisha anasafisha kuku. Kwanza anamchuna kuku kuondoa manyoya yaliyobaki katika nyama ya kuku. Baadaye, atamkatakata na kuanza kumpika.

Kwa kupika, wanatumia mkaa.

© African Languages Program, University of Georgia