Home
Overview
Technical Help

Select Unit > Unit 14: Mapishi > Lesson 2: Hide transcript

    

KWA CHAKULA CHA MCHANA FAMILIA YA BWANA MWISONGO WATAPIKA KAMA FAMILIA YA MZEE AYUBU.

Familia ya bwana Mwisongo ni kama familia ya mzee Ayubu. Wanawake wanatayarisha na kupika chakula chote. Wanasaidiana na wanazungumza wakati wa kupika. Ni wakati wa kufundishana mapishi pia.

Lakini familia ya Mwisongo inapata vifaa vya chakula chao kutoka mifugo yao na mashamba yao.

Kwa chakula cha mchana leo, watapika wali, mchuzi wa nyama ya ng’ombe, mchicha na njegere.

 

© African Languages Program, University of Georgia