Home
Overview
Technical Help

Select Unit > Unit 14: Mapishi > Lesson 3: Hide transcript

    

KUPAKUA CHAKULA NA KULA MKEKANI

Sasa chakula cha mchana ni tayari. Mama mwenye nyumba, yaani mke wake mzee Ayubu anakwenda jikoni kutazama mapishi. Kisha anaanza kupakua chakula na kuweka katika sahani, bakuli na sinia.

Kwanza anapakua kisamvu. Kisha anapakua sosi ya kuku na viazi.

Halafu anapakua wali. Kuna matandu juu kwa sababu alipalia mkaa juu ya mfuniko. Kwanza ataondoa matandu halafu ataupakua wali.

Sasa vyakula vyote ni tayari. Wanatayarisha mkeka chini wapate kula chakula cha mchana. Familia pamoja na wageni watakaa na kula pamoja.

© African Languages Program, University of Georgia