Home
Overview
Technical Help

Select Unit > Unit 14: Mapishi > Lesson 4: Hide transcript

    

FAMILIA YA MWINSONGO WANAKULA MEZANI

Sasa tunatembelea familia ya Bwana na Bibi Mwinsongo wakati wa asubuhi. Wao wanaishi Tanzania Bara karibu na mji wa Dar Es Salaam. Kabla ya watoto kwenda shule na wazazi kwenda kazini, wote wanakula chamshakinywa pamoja. Je, wanakula na kunywa nini? Wanakunywa chai. Wanakula mayai, chapati, na maandazi.

Kama katika familia ya Bwana Ayubu, katika familia ya Bwana Mwinsongo, wanakula pamoja. Lakini katika familia hii hawakai mkekani na hawali kwa mikono. Wanakaa mezani na wanakula kwa visu, uma, na vijiko.

© African Languages Program, University of Georgia