Home
Overview
Technical Help

Select Unit > Unit 14: Mapishi > Lesson 5: Hide transcript

    

KUPIKA MKATE WA UFUTA

Vifaa ni unga wa ngano, mafuta, tui la nazi, na chumvi.

Kutengeneza, Kwanza anachunga unga. Kisha anaweka hamira na tui la nazi. Anakanda unga na kuongeza tui la nazi mpaka unga umelainika. Anaupiga unga na kuukanda tena na tena ili kuongeza hewa katika unga.

Baada ya kunawa mikono, kusafisha sufuria na kusafisha sinia, anafunika unga kwa kutumia sinia.

Sasa Dada Zainabu anaanza kuchoma mikate. Kwanza kuchoma mkate wa ufuta. Anaweka chuma cha kuchomea juu ya mkaa na kukiacha mpaka kimepata joto. Kisha anachukua mchanganyiko kidogo na kuweka juu ya chuma. Anautandaza sehemu yote ya chuma cha kuchomea. Ananyunyuzia mbegu za ufuta juu na kuendelea kupika. Baada ya sehemu ya juu kukauka, anageuza chuma na kuchoma sehemu ya juu ya mkate kwenye mkaa. Baada ya kuiva, anautoa mkate na kuuweka katika sahani. Kisha anaupaka mafuta mkate ili usiwe mkavu sana.

© African Languages Program, University of Georgia