|
KUPIKA
MAANDAZI
Dada Zainabu anakanda unga wa maandazi. Vifaa vya kutengenezea
maandazi ni: unga wa ngano, hiliki, hamira, tui la nazi,na sukari.
Kwa kutengeneza: Kwanza anauchunga unga kwa kutumia chungio. Pili anachanganya unga, hamira, hiliki, sukari na tui la nazi. Kisha anaukanda unga, anaongeza tui la nazi na anakanda unga tena. Kisha anauacha mchanganyiko uumuke.
Sasa Dada Zainabu anaanza kutayarisha maandazi kwa kuchoma. Kwanza anaukanda unga tena. Anausukuma juu ya kibao. Anakata katika sehemu nne za kulingana. Anaviveka vipande juu ya ungo ulionyunyuziwa unga ili maandazi yasigande juu ya ungo. Baada ya kukata vipande vyote, anaviacha viumuke tena.
Sasa Dada Zainabu anachoma maandazi. Kwanza anachemsha mafuta katika kikaango. Ni lazima mafuta yawe yamepata joto sana. |