Home
Overview
Technical Help

Select Unit > Unit 15: Siasa > Lesson 1:

    

Chama cha TANU

Tanzania ilipata uhuru mwaka 1961. Kabla ya kupata uhuru, Tanzania ilikuwa koloni la Mwingereza. Mwalimu Julius Nyerere alikuwa raisi wa kwanza wa Tanzania. Ndiyealiyeanzisha chama ambacho kiliiletea Tanzania uhuru. Chama hicho kiliitwa TANU. Chama cha TANU kilizaliwa tarehe saba mwezi wa saba mwaka elfu moja, mia tisa hamsini na nne.

Ingawa chama tawala Tanzania sasa si TANU, kila mwaka wananchi wanasherehekea sikukuu hii ya kuzaliwa TANU na huitwa Saba Saba. Kazi zote za serikali husimamishwa na wananchi husherehekea kwa maandamano, ngoma, nyimbo na michezo mbalimbali.

Mwaka 1993, siku ya SABA SABA, wananchi walifanya maandamano pia. Lakini yalikuwa maandamano tofauti kwa sababu Tanzania imebadilisha muundo wake wa chama kimoja cha siasa kuwa muundo wa vyama vingi.

 

© African Languages Program, University of Georgia