Home
Overview
Technical Help

Select Unit > Unit 15: Siasa > Lesson 3: Hide transcript

    

  Kusoma Mashairi

  Vijana wa CCM wanasoma mashairi ya kusifu chama tawala cha CCM.
  =================================

  Yavutia Tanzania

  Tanzania kuna watu wema wasio kifani
  Watu wanajali utu tena wapenda amani
  Ni watu wenye hekima wanajua ya usoni
  Uliza dunia nzima kaulize Marikani
  Sema taifa gani la watu wenye huruma
  Watasema Tanzania

  Tanzania kuna mito ya chini na milimani
  Kuna mawe ya kokoto yaliyobaki yawe madini
  Tena kuna mbuga zetu zasikika duniani
  Halafu kuna mlima wa kwanza Afrikani
  Nasemwa bandarini njema kwenye ukanda wa pwani
  Iko hapa Tanzania

  Ni nchi yenye hakika hasa swala la amani
  Asubuhi ikifika utaiona jioni
  Tabia ya kupigana Tanzania haiendani
  Tanzania tumepatana sisi hatujali dini wala rangi
  Rangi wala jinsia
  Sisi tunavyoamini, mweusi au mweupe
  Wote ni Watanzania.

  Watakao kutugawa kwa rangi au kwa dini
  Hao wamepungukiwa ni sawa na punguani
  Hawafai Tanzania
  Naona nikae nchini
  Muda nawaachieni
  Maswali niulizeni.


© African Languages Program, University of Georgia