Home
Overview
Technical Help

Select Unit > Unit 15: Siasa > Lesson 5: Hide transcript

    

Hotuba ya siasa

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, ndugu Kolimba, anasoma risala kwa makamo wa kwanza wa rais, ndugu Salmin Amour.

Ndugu makamu mwenyekiti wa chama cha vijana, ndugu wajumbe wa kamati ya taifa, waheshimiwa mawaziri, waheshimiwa wabunge, wanachama wa chama cha mapinduzi (CCM), wakereketwa wa chama cha mapinduzi, wapenzi wa CCM wote, washabiki na umma wa mkoa wa Dar Es Salaam, mabibi na mabwana.

Ndugu makamu, awali naomba uniruhusu kwa niaba ya uongozi wa CCM, wanachama na uma wa mkoa wa Dar Es Salaam nikushukuru sana kwa kukubali kwako kuja na kushirikiana pamoja nasi katika matembezi haya muhimu ya mshikamano siku hii ya leo.

Ndugu makamu, kushiriki kwako katika matembezi haya ya mshikamano hapa Dar Es Salaam kumekiongezea haiba, uhai, na nguvu, chama cha mapinduzi hapa mkoani.

Aidha, ndugu makamu, tunaishukuru kwa dhati kamati kuu ya halmashauri kuu ya taifa kwa kukupanga wewe, nguzo ya siasa, chimbuko la mageuzi, mpenda maendeleo, na mkereketwa wa dhati wa CCM, kuja kutembea na sisi hapa Dar Es salaam. Tunasema makamu, asante sana na karibu mkoani Dar Es Salaam.

 

© African Languages Program, University of Georgia