|
Risala Kutoka Chama cha Vijana
Msafara wa
wapanda pikipiki.
Walitembea katika vijiji mbalimbali kueneza siasa ya Chama cha CCM.
Sasa wapanda pikipiki wanasoma risala yao kwa makamo wa kwanza wa raisi na mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Dar es Salaam.
Tumetembea mikoa ishirini ya Tanzania Bara, kwa nia ya kuwaomba Watanzania kudumisha
amani, upendo na mshikamano bila ya kujali itikadi zetu za kisiasa. Tuliwakumbusha wananchi kwamba, kwenye vita hapana siasa na haki nyingi za kiraia hupotea. Hivyo
tumewaomba Watanzania kujenga utamaduni wa amani, upendo na mshikamano katika nchi yetu.
Ndugu mwenyekiti, msafara wetu umepata mapokezi makubwa kwa wananchi, viongozi wa
mkoa, wilaya, chama na serikali katika maeneo tuliyopita.
Ndugu mwenyekiti, msafara wetu ulizinduliwa tarehe kumi, mwezi wa sita, mwaka
elfu moja mia tisa tisini na tatu katika shina la wakereketwa,
Buguruni. Akizindua msafara
huu, katibu mwenezi
wa chama cha mapinduzi, ambaye pia ni waziri asiyekuwa
na wizara maalum,
ndugu Kingunge Ngombale Mwiru, amesifu juhudi zako
za kudumisha amani, upendo, na mshikamano ambao kwa kiasi kikubwa umesaidia kujenga
utulivu nchini. Pia ametutaka sisi wapanda pikipiki kuwa jasiri ili kuweza
kufanikisha safari yetu.
Ndugu mwenyekiti, msafara wetu baada ya kuzinduliwa, umepitia maeneo yafuatayo - Kilwa Masoko, Kilwa Kivinje, Iringi, Mtwara, Masasi,
Tunduru, Songea, Makambako, Mbozi, Mbeya, Tuduma, Sumbawanga, Mpanda, Kigoma, Kibondo, Kasulu, Biharamulo, Muleba, Bukoba,
Mwanza, Shinyanga, Nzega, Tabora, Itigi, Manyoni, Dodoma, Kondoa, Arusha, Moshi, Tanga, Muheza, Chalinze, Kibaha, na Dar Es Salaam.
Msafara wetu ulichukua siku ishirini na tatu.
|