Home
Overview
Technical Help

Select Unit > Unit 17: Utalii > Lesson 1:

    

Mbuga za Manyara I

Wageni wengi wanaokuja Tanzania wanapenda kutembelea mbuga za wanyama. Tanzania imebarikiwa kwa wanyama wa kila aina. Kuna mbuga kubwa tatu ambazo Tanzania imehifadhi wanyama mwitu. Mbuga hizi ni Mikumi, Manyara na Serengeti. Mbuga hizi zinatunzwa na wafanyi kazi wa wizara ya Utalii na Mali Asili,Tanzania. Tutatembelea mbuga za Manyara na Mikumi. Kwanza mbuga za wanyama Manyara. Mbuga za wanyama Manyara ziko katika jimbo la Arusha, kaskazini Tanzania. Watalii wanaozitembelea mbuga hizi hukaa katika hoteli ya Manyara. Wizara ya Utalii inawapatia watalii viongozi ambao ni wataalamu wa wanyama mwiti. Viongozi hawa wanawaongoza watalii katika mbuga hizi na kuwaonyesha wanyama mbalimbali.

Huyu ni kima. Kima anapenda kukaa karibu na njia. Kuna matangazo kwa watalii. Wanaombwa kutowalisha chakula cho chote kima hawa.

Huyu ni fisi.

Hawa ni pundamilia.

Hawa ni nyumbu.

Hawa ni simba: simba dume na simba jike. Wamemaliza kula na sasa wana usingizi.

Huyu ni pongo.

Huyu ni tai. Hukaa karibu na mahali penye mzoga wa mnyama ambaye ameuawa na simba au chui.

Hawa ni kima Wengine. Kima wanapenda kukaa karibu na njia.

Hii ni familia ya swala.

Huyu ni tembo.

© African Languages Program, University of Georgia.