Home
Overview
Technical Help

Select Unit > Unit 17: Utalii > Lesson 2: Hide transcript

    

Mbuga za Manyara II

Hii ni familia ya twiga. Kwa sababu ya shingo zao ndefu, wanaweza kula majani ya juu kabisa katika miti. Majani haya ni laini.

Huu ni msafara wa nyumbu. Kwa kawaida wanakaa kwa kikundi ili kujilinda.

Huyu ni tembo. Anatumia mguu wake kukusanya majani, mkonga wake kuweka majani mdomoni na pembe zake kujilinda.

Hawa ni nani?

Huyu ni mama tembo na mwanawe.

Maji haya yanatoka chini ya ardhi. Kwa sababu ya nguvu na joto la volkeno katika sehemu hii, maji haya ni moto sana.

Hili ni ziwa Manyara. Ndege kama mbuni na wanyama hufika kunywa maji na kuogelea.

Hawa ni nani? Kima na watoto wake.

Hii ni familia ya kiboko, baba, mama na mtoto.

 

© African Studies Institute, University of Georgia