Home
Overview
Technical Help

Select Unit > Unit 17: Utalii > Lesson 3:

    

Magofu ya Kaole - Bagamoyo

Makumbusho ya historia ya watumwa yanaonekana sehemu za Bagamoyo pia. Sasa tutatembelea magofu ya Kaole katika wilaya ya Bagamoyo. Magofu haya bado yanachunguzwa na wataalamu wa akiolojia.

Serkali bado inayalinda magofu haya. Kwa hivyo hapa pana mlinzi wakati wote. Mlinzi wa kituo hiki na magofu haya anapendelea kujulikana kama Profesa. Kwa jina kamili basi ni Profesa Samahani Kejeli. Profesa Kejeli atatueleza kwa kifupi juu ya magofu haya.

Historia yetu kabla hatujaelezana, kuna tangazo muhimu. Hili tangazo ni kwa kila mgeni wetu lazima aanze kulifahamu hili kwa sababu kuta zetu ni nzee sana. Kwa hiyo karibuni sana tuanzie hapa.

© African Languages Program, University of Georgia