Home
Overview
Technical Help

Select Unit > Unit 17: Utalii > Lesson 5: Hide transcript

    

Kupumzika pwani

Kwa kujistarehesha, watu wanaokaa karibu na pwani hupendelea kwenda pwani kupumzika. Hii ni bustani ya mapumziko kisiwani Unguja karibu na bandari ya Zanzibar. Watu wengi wanavutiwa kupumzika katika bustani hii. Kwa hivyo, wafanyi biashara wadogo wadogo wanatumia nafasi hii kukuza mitaji yao. Wanawauzia wapumzikaji vitafunio mbalimbali. Kwa mfano: mishikaki, miwa, mihogo ya kuchoma au kukaangwa, pweza wa kuchomwa, viazi vya kuchomwa au kukaangwa, maji ya matunda na kadhalika. Kama tunavyoona watu huenda pwani kupumzika, kuzungumza, kutazama boti na meli zinazokwenda majini na kupunga upepo.

© African Studies Institute, University of Georgia