|
SOKONI ZANZIBAR
Katika somo la leo tutatembelea masoko. Kwa kawaida masoko ya Afrika yanafanana sana. Huwa nje katika sehemu ya wazi na watu wanaweza kupata vyakula mbalimbali kutoka sehemu mbalimbali za nchi.
Kwanza tutatembelea soko la mjini Zanzibar. Kwa sababu ya utamaduni, mila na desturi za wenyeji wa Unguja, wanaume zaidi ya wanawake huenda sokoni kuuza na kununua vyakula.
Tunaweza kuona nini sokoni hapa? Matunda mbalimbali kama mafenesi, mashelisheli, mabungo, maembe, mapapai, ndizi, ukwaju, mananasi, nazi, ndimu, machungwa, machenza. Mboga kama: kisamvu, mchicha, biringani, nyanya
mviringo, nyanya
mshumaa, maboga bamia.
Nafaka kavu kama: maharagwe, zabibu
kavu, choroko.
|