|
MAZUNGUMZO
NA MWUZAJI WA MATUNDA
Kama unakaa mjini Dar es Salaam au katika viunga vya mji si lazima
kwenda sokoni Kariakoo
kupata mahitaji yako.
Soko la Kariakoo ni soko kubwa mjini Dar
es Salaam lenye bidhaa mbali
mbali. Lakini watu wengi wanapenda masoko madogo
madogo katika mitaa mbali mbali ya mji. Tutembelee sehemu
moja karibu na barabara kuu
ya Bagamoyo.
Msaili: Hujambo bwana.
Mwuzaji: Sijambo. Hali yako.
Msaili: Nzuri, na wewe.
Mwuzaji: Salama.
Msaili: Unaitwa nani?
Mwuzaji: Kwa jina naitwa Omari Hassan.
Msaili: Omari Hassan. Mwenyeji wa wapi? Ndugu yangu?
Mwuzaji: Mimi Mwenyeji wa wilaya ya Kisarawe.
Msaili: Sasa unafanya nini hapa?
Mwuzaji: Nauza matunda.
Msaili: Matunda? Mnayapataje haya?
Mwuzaji: Haya matunda tunayapata kutoka mkoa wa pwani, Dar es Salaam na Kilwa rodi.
Msaili: Kilwa rodi sehemu gani?
Mwuzaji: Mkoa wa pwani sehemu za Kimasichana.
Msaili: Mnakwenda kuchukua wenyewe?
Mwuzaji: Wenyewe tunakwenda kuchukua na mengine tunanunua sokoni Tandika.
Msaili: Kwa hivyo kutokana na biashara hii ndiyo unapata ile kula yako ya kila siku?
Mwuzaji: Sawa
sawa.
Msaili: Na inatosheleza?
Mwuzaji: Inatosheleza kwa sababu binadamu hatosheki.
Ukitaka kutosheleza moja kwa moja, inakuwa ngumu. Lakini kiasi kwamba inaleta manufaa.
Msaili: Kwa hiyo familia yako haina matatizo. Na msimu ambao huna matunda
unafanya nini?
Mwuzaji: Huwa Tunafuatilia tunda
hadi tunda. Tukitoka kwenye machungwa
tunaingia kwenye zabibu, mananasi, maembe, mapapai, ndizi.
Msaili: Kwa hiyo mwaka mzima unashughuli ya kuuza matunda?
Mwuzaji: Matunda tu.
Msaili: Na haya unauzaje?
Mwuzaji: Hapa tano, kumi, kuna ya ishirini.
Msaili: La shilingi tano ndo lipi. Hebu nionyeshe. Hili ndio shilingi tano?
Mwuzaji: Shillingi tano.
Msaili: Na lingine?
Mwuzaji: Hili shilingi kumi.
Msaili: Kwa hiyo mnajua kuyapanga kwa saizi mbalimbali.
Mwuzaji: Eeh.
Msaili: Na una mashine ya kuchagua au wewe mwenyewe tu?
Mwuzaji: Mimi mwenyewe tu. Si uzoefu?
Msaili: Haya
bwana.
|