Home
Overview
Technical Help

Select Unit > Unit 18: Biashara > Lesson 3: Hide transcript

    

ZAO LA KAHAWA

Katika mashamba ya Tanzania kuna mazao ya chakula na mazao ya biashara. Kahawa ni zao muhimu la biashara pia. Sasa tutatembelea shamba la kahawa huko kaskazini ya Tanzania, miji ya Moshi na Arusha. Sasa tutaona hatua za kahawa tangu mche hadi mbegu ya kahawa kavu. Kwanza mbegu zinaoteshwa katika vitalu. Baada ya miche kuwa na urefu wa kutosha, inaoteshwa katika umbali wa futi tatu. Baada ya mwaka mmoja au miwili, mche unatoa matunda ya kahawa. Baada ya ya matunda haya kuiva, yanachumwa. Halafu yanasagwa katika mashine maalumu kuondoa maganda. Kisha mbegu zinawekwa kwa siku tatu au nne ili kuchacha. Baadaye zinasafishwa na kuanikwa juani mpaka zinakauka kabisa. Kisha mbegu zinawekwa katika magunia na kuuzwa kiwandani.

Katika kiwanda, wanakoboa maganda ya nje na kupata mbegu ya ndani. Mbegu hii hukaangwa na kusagwa tayari kwa kutengeneza kikombe cha kahawa. Kahawa inaweza kuuzwa nchi za nje kama mbegu kabla au baada ya kukaangwa na kusagwa.

 

© African Studies Institute, University of Georgia