Home
Overview
Technical Help

Select Unit > Unit 18: Biashara > Lesson 4: Hide transcript

    

ZAO LA MKONGE

Zao jingine la biashara Tanzania ni mkonge. Nyuzi za mkonge zinaitwa katani. Unaweza kutumia nyuzi za katani kutengeneza magunia ya kusafirishia mazao mbalimbali.

Sasa tunatembelea shamba la mkonge na kiwanda cha kutengenezea nyuzi za katani. Sasa tutaona hatua za katani tangu mche hadi katani kavu. Hili ni shamba la mkonge na huu ni mkonge mchanga shambani. Sasa tunaona mkonge uliokomaa. Sasa mkonge unakatwa na kuwekwa katika matoroli. Sasa mkonge unasagwa ili kupata nyuzi. Sasa nyuzi zinatolewa, zinaoshwa na zinaanikwa. Sasa nyuzi zinakusanywa na kufungwa katika mafungu. Haya ni marobota ya katani tayari kuuzwa nchi za nje.

 

© African Studies Institute, University of Georgia