KIKUNDI CHA TANZANIA Msaili: Haya kikundi chenu hiki. Nitataka kujua kama mna maduka kule mjini. Shughuli zenu za ni ni akina mama eh?
Mfanyibiashara: Eh, ni kundi cha akina mama.
Msaili: Ehe.
Mfanyibiashara: Tuko watu kama
sasa hivi tumeshafika kumi.
Msaili: Ehe.
Mfanyibiashara: Na tulianza kwa mtaji kidogo kidogo. Tulianza hamsini
elfu kila mmoja. Tukaona hautoshi. Tukaongeza mpaka
tukafika laki moja. Tukaona tulipoingia katika maonyesho ya
mwezi wa nne haikutosha. Kwahivyo tukaanza
mpaka tukafika laki
moja unusu kila mmoja. Baada ya hapo tukaanza kutengeneza batiki hizi wenyewe
na wengine tukazunguka mikoani kuweza
kupata vitu vichache vichache ambavyo ni hendikrafti zinazotengenezwa
na wakina mama. Vingi vilikuwa vimetoka mkoa wa Iringa kama vikapu unavyoviona
pale. Halafu na vingine vya Dodoma. Kwahivyo tukaenda kule tukakaa na grupu za
akina mama tukajaribu kuwapa
moyo watengeneze quality ambayo itakuwa ni nzuri kwa ajili ya kuexport nje. Kwahivyo
tumejaribu kuwasiliana nao
mpaka tukaweza kuingia katika mashindano.
Na lengo letu
kuu hasa ni
kuweza kuwavuta wale akina mama hasa kwenye rural area waweze kujimudu wenyewe
watengeneze vitu vyao ambavyo viko kwenye uwezo wao bila ya kutegemea material
kutoka nje, au nini. Na sisi tukiweza kupata msaada wa kuvipeleka nje
ili tuweze kuinua hali yao. Kwa hivyo integration iko kutoka kwa wanawake wa
kijijini mpaka sisi ambao tumeanzia hapa mjini.
Msaili: Je, mnayo maduka ya kusambazia vitu
vyenu hivi hapa mjini Dar es Salaam au mikoni?
Mfanyibiashara: Sasa hivi tuna duka moja. Bahati nzuri
tumepata ofisi mtaa wa
Kariakoo, mtaa wa Nyamwezi na Lindi strit, kuna baa moja imeandikwa Furahia Baa.
Upande mmoja wametupa ndo tumefanya ofisi na duka. Kwahivyo tuna ofisi na duka
sasa hivi.
Msaili: Je, hapa kuna nguo za akina nani? Akina mama, watoto, au nguo
gani hasa ulizo nazo hapa?
Mfanyibiashara: Kwa
kweli nguo zetu hapa tuna nguo za wakina mama, tuna nguo za watoto wa kike, tuna
nguo za akina baba na aina nyingi ni batiki. Japo chache tulikuwa na vitenge tumenunua ambavyo sasa hivi tunatarajia. Tunafanya seli leo ili watu waweze kununua na tumefanya seli ya rahisi sana utakuta sketi na blauzi shilingi elfu tano na quality moja yetu ya hivi vitu vyetu iko katika finishing. Ile finishing yake ni nzuri sana. Na nguo za akina baba ziko pale ambazo tumetengeneza mashati na nguo nyingine za kuvaa.
Msaili: Asante sana. Tunashukuru sana. Na tunakutakia kilala heri katika mafanikio yenu
ya hasa kuwaunganisha kina
mama. Mfanyibiashara: Karibuni sana.
Msaili: Asante.
Mfanyibisahara: Asante sana.
|