MAONYESHO YA KANGA NA VITENGE Je, wanapata nguo hizi kutoka wapi?
Baadhi ya vitambaa vinatoka nchi za nje kama Afrika ya Magharibi, Afrika ya Kati, na hata sehemu za Asia na Ulaya. Pia vitambaa vingine vinatengenezwa katika viwanda vya hapa Tanzania. Twende kwenye banda la kanga na vitenge kutoka viwanda vya hapa nchini Tanzania.
Hizi ni kanga. Kanga huvaliwa na akina mama zaidi.
Akina baba je? Akina baba wanaweza kuvaa kanga nyakati za jioni wakati wa mapumziko na hasa wakati wa joto. Hujifunga kiunoni na kuvaa shati juu yake.
Kwa akina mama, matumizi
ni mengi sana. Wanaweza kujitanda,
kujifunga, kuvaa kama vazi rasmi, kubebea watoto
mgongoni na kufungia mizigo.
Hivi ni vitenge. Hutumiwa kushonea mavazi mbalimbali kwa watoto, akina mama na wanaume pia.
Hizi ni kanga nyingine. Rangi zake zinapendeza machoni.
Kweli. Na zote hizi zinatengenezwa hapa Tanzania katika viwanda vya Urafiki, Mwatex, Sunguratex na Kiltex.
|